Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TEST 14

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A (Alama 20)

Riwaya
1.

a) (i) Mzungumzaji ni Mtemi Nasaba Bora.

(ii) Anamwambia mwalimu Majisif Majimarefu.

(iii) Wako nyumbani kwa Mtemi Nasaba Bora.

(iv) Mwalimu alikuwa amemtembelea akiwa na dukuduku moyoni lakini hakumfahamisha aliyokuwa nayo.(1x4=4)

b) Mwalimu ana dosari zake mfano;

―Ulevi wa kupindukia.

―Kunywa pombe haramu/duni-‘gongo’.

―Kuzembea kazini-kutokwenda shule.

―Kutowajibikia malezi.(zozote 3x1=3)

Mtemi Nasaba haoni dosari zake mfano;

―Mapenzi na wasichana wadogo-Lowela.

―Ufisadi,unyakuzi wa mali.

―Kutoa hongo(mahakama,polisi,jeshini).

―Kutotunza mandhari ya nyumbani,kasri.

―Utawala mbaya, udhalimu.

―Kuupuza malezi ya mashaka,madhubuti pia anaasi(zozote 3x1=3)jumla 6

c)Sadfa

i. Sadfa ni matukio mawili au zaidi kutokea wakati mmoja bila kupagwa.

ii. Amani kukutana kisadfa na Imani pale Ziwa Mawewa,Imani akitaka kujuwa na kughairi nia.

iii. Imani na Amani wote kuharibikiwa na kwao kutaka tama-Amani kutaka kujitosa na Amani kutaka kuutosa mswada majini.

iv. Amani na Imani kukutana ba DJ,BOB,katika mto Kiberenge-baadaye anawaeleza kupata ajira.

v. Amani na Imani kuajiriwa na ndugu wawili

-kazi ngumu-kukoma na ujakazi.

vi. Baada ya majisifu kubishana na Dora kuhusu ubingwa wake uandishi analetewa barua na Mashaka ya ulioishi huko mkokotoni.

vii. Wakati Zuhura anamwalika Amani chumbani ndipo Nasaba bora arudi na kuwafumania.

viii. DJ kupitia karibu na kibanda cha Amani wakati Amani anawaza atafanya nini na kitotoAnamtuma DJ kwa Imani aje amsaidie.

ix. Amani anapitia pale ambapo Oscar Kambona(Gadaffi)anataka Kumuua Mtemi Nasaba Bora-anamuokoa. x. Vitabu mojawapo anavyopewa Amani kusoma pale kwa majisifu ni kidagaa kimemwozea ambacho ni chake.(zozote 5x2=10)

Tanbihi*mwanafunzi akitoa mifano mingine inayofaa atuzwe.

20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

Tamthilia
2.

MSTAHIMIKI MEYA-Timothy Areg

i. Mhusika Nguli ni mhusika anayewakilisha mama katika jamii na hutetea umma.

ii. Mtetezi wa Haki(wafanyikazi,wagonjwa)

iii. Mwajibikaji (Hospitalini,kujali wagonjwa)

iv. Mshauri mzuri(Anawashauri Meya,Diwani III,Waridi,Tatu)

v. Mvumilivu/subira-kazi katika mazingira magumu lakini anaendelea-ukosefu wa dawa.

vi. Mzalendo dhabiti/mzalendo chonya-kukataa shirikizo za kigeni,kutaka maendeleo,kupinga ndugu yake.

vii. Uadilifu –kuzingatia maadili ya kikazi/taaluma.(zozote (5x2=10)

Meya Sosi.

i. Mhusika hasidi ni anayewakilisha uovu,katika Jamii-anadhulumu umma,ni adui wa nguli.

ii. Mlafi –(meza imejaa vyakula vingi-analalamikia viyai ilhali watu wengine wanakosa chakula na kula uporo.

iii. Mapuuza –kupuuza madai ya wafanyakazi.

iv. Katili –anadai kifo ni cha mtoto mmoja tu!

v. Mbinafsi –anaagiza maji yake pekee,kujilimbikizia mali,vyakula vingi kwake.

vi. Tamaa-(ya mali,ardhi,cheo)

vii. Udikteta –mabavu,hakubali maoni ya wengine ,amri ya nyongeza ya mishahara kwa madiwani,mkali kwa Gedi,Dida,Askari.

viii. Mbadhirifu –kupeleka mkewe matibabu ng’ambo,wanawe kusomea ng’ambo,hoteli za kifahari.

ix. Fisadi-(kandarasi,ardhi,fimbo,kulipa Bili,kuajiri mhazili)

x. Vitisho –(kufuata kazi wafanyakazi,kumtisha Siki,kutisha Diwani III)

xi. Laghai (kudanganya wafanyakazi,umma,kuhusu dawa)

xii. Mnafiki –(kujifanya mcha mungu,mpole,kuwaalika viongozi wa wafanyakazi hila) (zozote 5x2=10)

3. a) ―Msemaji ni Dkt Siki.

―Anamwambia Waridi.

―Wako Zahanatini.

―Wanazungumzia kukosekana/kuchelewa kwa dawa kwamadai kuwa ziko njiani lakini Siki anajua kuwa huo ni uongo mtupu.(zozote 4xz1=4)

b) ―Siki amepevuka kimawazo-anatambua uongo wa Meya na wenzake.

―Mtetezi wa haki-dawa zinapokosekana anaamua kwenda kuonana na Meya mwenyewe.

―Mwenye utu na huruma-anawahudumia wagonjwa japo hakuna dawa hata wanapokosa pesa anawahudumia na kumwagiza Waridi awalaze. ―Hakati tamaa-baada ya kukaa na kuwahudumia wagonjwa bila dawa Waridi anajiuzulu lakiniSiki anaamua kuendelea kuwapa wagonjwa matumaini. ―Mshauri mwema-anampa Meya mashauri ambayo yangeboresha utawala wake japo hamsikilizi wala kumthamini.(zozote 3x2=6)

c) ―Ukosefu wa chakula-wanakula makombo kutoka kwa Meya.

―Vifo- kutokana na ukosefu wa dawa na chakula k.v binamuye Waridi.

―Mishahara duni-wafanyakazi hawamudu huduma za matibabu wala lishe bora.

―Mishahara kuchelewa-kwa miezi mitatu.

―Mazingira machafu-kila pahali kumejaa uchafu barabarani, hospitalini.

―Elimu duni-Meya na wenzake wanapeleka watoto ng’ambo kusomea huko.

-Dhuluma-wanyanyakazi wanapogoma wanachapwa na askari.(zozote 5x2=10)

20 marks

SEHEMU YA C (Alama 20)

Ushairi
3.

4. a) Takriri/uradidi mf

Taathira

Taathira


Ardhi

Ardhi
Mwanzo

Mwanzo
Mirathi

Mirathi. n.k
Kutaja 1 =Mfano 1 =2

b) (i) Beti zina mkondo sawa.

(ii) Idadi ya mizani kati ya Beti ni sawa.
(iii) Kuna urari wa vina katika mistari ya Beti.

(iv) Shairi lina kibwagizo.

(v) Kuna migao sawa(ukwapi na utao)-mathnawi.

(vi) Inazingatia Bahari maalum-ukaraguni,msuko,tasbia,mathnawi. (zozote 4x1=4)

c) (i) Inkisari- mifano ‘Liandama,warinasi,inonuka,zilopapangwa,yali,Iso. Sababu-kusawazisha mizani,kuleta mdundo.

(ii) Mazda-kupituka,Ardhi. Sababu-kusawazisha mizani,mapigo ya sauti.

(iii) Tabdila-hefika-mapigo ya sauti.

(vi) Kufinyanga sarufi- (kuboronga sarufi)-

mf langu jicho,changu kinywa Sababu

–kuonyesha ufundi,mapigo ya sauti. (zozzote 3x2=6)

Kutaja + mfano-1 Sababu -1

d) Wanategemea mazingira na yanapoangamia hakuna anayejali/ingawa miti ina faida ya siku za usoni.(1x2=4)

e) (i) Kibwagizo kimerudiwa-msisitizo.

(ii) Kimefupishwa-msuko.

(iii) Uakifishi(alama hisi)-msisitizo.

(iv) Kiini.(zozote 2x2=4)

f) (i) Mazagavu-yaliyoenea kote.(1x1=1

(ii) Majilisi-makao (1x1=1)

5. a) Umuhimu wa miti/faida ya miti/utunzaji misitu n.k(1x2=2)

b) (i) Beti zinachukua mikondo tofauti tofauti.

(ii) Hakuna urari wa vina.

(iii) Idadi ya mizani inatofautiana kila mshororo na Beti.

(iv) Beti hazina vibwagizo ni vimalizio/viishio.

(v) Umbo la ajabu(mambo ya vitu halisi)ni sifa ya mashairi huru/kisasa.

(vi) Idadi tofauti ya mishororo kila beti.(zozote 4x1=4)

c) Kuelimisha juu ya umuhimu wa miti/faida za miti kukashifu wasiojali miti/mazingira.(4x1=4)

d) Mwanadamu anapoathiriwa na magonjwa mbalimbali,suluhisho ni matibau mwafaka.Matibabu haya hupatikana kutoka kwa miti kwa kutumia madawa yanayofaa mwanadamu anaweza kuokoa maisha.(4x1=4)

e) Hewa nzuri tupatayo,maji safi tutumiayo hata mandhari yawayo,n.k.(2x1=2)

f) Mti.(1x2=2)

g) (i) Balagha - si heko kwa miche?

(ii) Taswira - mti uchipukao.

(iii) Takriri - Yo,Yo,Yo, ubeti 8, 9 2x1=2 Kutaja ½ Mfano ½

h) Kiulizi

- (i) Kusisitiza ujumbe.

(ii)Kubainisha balagha (yoyote 1x2=2)

20 marks

SEHEMU YA D (Alama 20)

Damu nyeusi na hadithi nyinginezo
4.

6. Damu nyeusi.

a) -Ni mawazo ya Fikirini.

-Alikuwa chumbani kwa Fiona na Bob.

-Fiona alimlaghai kwamba angemfaa kumbe alitaka kumpeleka kwa jambazi mwenzake Bob.
-Anayawaza maneno haya akiwa amefungiwa chumbani akiwa uchi analia kama mtoto kwa uoga.(zozote 4x1=4)

b) -Takriri

– siku ya siku.

-Msemo

–siku ya siku.

-Methali – siku ya nyani kufa,miti yote huteleza.(zozote 2x2=4)

c) -Ubaguzi wa rangi uliomtia huzuni na upweke kule ughaibuni.

-Maswali ya kukera kwa sababu ya mwelekeo hasi wa wazungu kwa wafrika.

-Fikirini anaachwa na dereva wa basi kwa kuwa Mwafrika.

-Wahadhiri chuoni wanawatuza wanafunzi weupe alama za juu.

-Sheria ya nchi iliendeleza ubaguzi –Fikirini alitozwa faini na polisi lakini watu weupe wakaachwa.

-Anatuhumiwa kuwa mwizi- madukani anafuatwa fuatwa.

-Anaposahau kufunga zipu ya suruali yake,anaitiwa polisi wanaomkabili kwa bunduki.

-Anapigwa na kuporwa kila kitu na Wamerakani weusi aliodhani ni nduguze-Fiona na Bob.(zozote 6x2=12)

20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

Fasihi simulizi
5.

FASIHI SIMULIZI

a) Ngomaz ni Fasihi ya ngoma ambapo makabila mbalimbali huwasiliana kutumia milio ya ngoma na ala zingine za muziki bila kutumia maneno.(1x2=2)

b) Sifa za ngomaz.

-Hufumba ujumbe fulani kwa wasiohusika.

-Hushirikisha zana za muziki zenye mapigo maalum.

-Ujumbe wa ngoma hufasiriwa na wanajamii kama wanavyokubaliana awali.

-Hutoa ujumbe mzito,maalum na wa dharura kwa njia nyepesi,rahisi na haraka.

-Hutekeleza majukumu ya maandishi katika jamii.(zozote 5x2=10)

c) Umuhimu wa Ngomez.

-Hutoa taarifa kwa njia rahisi na kuwafahamisha wanajamii juu ya tukio lolote.

-Hutahadharisha jamii juu ya dharura au hatari yoyote kwa haraka.

-Hudumisha na kurithisha utamaduni wa jamii.

-Hudhihirisha ufundi wa kisanaa katika uchezaji zana za muziki.

-Husaidia katika sehemu zilizo na mawasiliano magumu.(zozote 5x1=5)

d) Udhaifu.

-Mabadiliko ya hali ya anga huathiri mawasiliano.

-Huweza kutumika tu katika masafa ya karibu.

-Inahitaji ufundi maalim kucheza ala.

-Hakuna njia ya kudhibiti sauti isiwafikie maadui.(zozote 3x1=3).

20 marks

Back Top