Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 15

Kiswahili Paper 2

1. UFAHAMU (Alama 15)

Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali.
1.

a. Shambulizi la kigaidi Ugaidi Shambulizi la Westgate Mkasa wa Westage (1 x 1 =al.1)

b. (i). Watu 67 waliaga dunia

(ii).Wengine 175 waliachwa na majeraha mengi. (2 x 1 = al. 1)
c. (i). Kinaya ni kwamba mawaziri wanne na maafisa wa usalama nchini walipashwa habari za kijasusi kuhusu mipango ya magaidi kutekeleza shambulizi lakini viongozi hao hawakuchukua hatua za kuzuia shambulizi hilo.

(ii). Wachunguzaji wa ujasusi walikuwa hatika kituo hicho masaa machache kabla ya magaidi hao kufika na kuanza kufyatulia risasi walinda usalama na raia lakini hawakuweza kugundua ili kuzuia.

(iii). Wachunguzaji waliwasiliana na maafisa wa polisi wanaoshika doria mara kwa mara katika kituo hicho kabla ya shambulizi kutekelezwa. (2 x 2 = al. 4)

d. (i). Kwamba wao wamezembea katika majukumu yao ya kuwahakikishia wakenya na wageni wanaozuru Kenya usalama.

(ii). Wanastahili kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuzembea kazini. (1 x 2 =al.2)

e. Vitisho kuwa magaidi wanapanga kutekeleza mashambulizi mengine. (1 x 2 =al.2)

f. Serikali inapaswa kutumia shambulizi la Westgate kama funzo litakalozifanya idara zake za usalama kuamka usingizini na kuhakikisha kwamba wakenya hawapotezi maisha yao tena katika visa vya ugaidi. (1 x 2 =al.2)

g. (i). Kuchukua jukumu la kuwajua vyema majirani zao na kuripoti jambo lolote lisilo la kawaida kwa maafisa wa usalama.

(ii).Waweze kushikana mikono na polisi katika kuwakamata watu wenye nia mbaya mitaani na kuwachukulia haatua za kisheria. (2 x 1 = al. 2)
Jinsi ya kutuza

-Ondoa ½ alama kwa kosa la sarufi litokeapo mara ya kwanza kwa kila kijisehemu. Usiadhibu zaidi ya nusu alama alizozipata katika kijisehemu hicho. -Ondoa ½ alama kwa kosa la tahajia litokeapo mara ya kwanza hadi kufikia makosa 6.

15 marks

2. UFUPISHO (Alama 15)

Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali yanayofuata.
2.

(a). -Utando wa ubongo (meningitis) huzua hofu.

-Huathiri ngozi inayofunika ubongo.

-Bakteria huwa hatari kuliko virusi kwa kusababisha meningitis.

-Wagonjwa wengi watibiwapo haraka hupona lakini wengine huachwa wakiwa bubu au vipovu na wengine hufariki.
-Ripoti hii ni kwa mujibu wa wataalamu wa afya. Zozote 7 ala 7 (mtiririko 1)

(b). Dalili

-Watoto hupatwa na homa, hutapika, kukataa kula na kulia kwa uchungu.

-Aidha kufura kichwa, kupumua kwa haraka, kutupatupa miguu na mwili kujikunyata.

-Watu wakubwa hupatwa na maumivu makali ya kichwa na shingo nzito.

-Wao hutapika na kukosa ufahamu.

-Aidha hupatwa na mikono na miguu baridi,maumivu ya misuli na tumbo kutokana na damu kuwa na sumu. Hatua:- Mhasiriwa yeyote anayeshukiwa apelekwe hospitalini maramoja.

M a -7

b -6

ut -2 = 15

Makosa s-makosa 6 (al. 3)

h- makosa 6 (ala.3)

15 marks

3. MATUMIZI YA LUGHA (Alama 30)

3.

(a). (i) LI –YA

Pera mapera (Alama 1)

(Sentensi lazima idhihirishe upatanisho wa kisarufi katika ngeli ya LI-YA)

(ii). Kitone Mwishoni mwa sentensi Kuandika maneno kwa kifupi Kutenganisha fedha (Ataje hoja na kutoa mfano) hoja½ mfano½

(Alama 3) (b).

Wakati –PO Mfano –wageni walipowasili wanafunzi walishangilia. (Alama 1)

Mahali - Po ko mo + ni -Mle sandukuni mna nguo -Kule alikozaliwa kumelimwa (Alama 1)

Namna –Ki-Vi Alijeruhiwa vibaya Mwizi alipigwa kikatili/kistadi (Alam 1)

(c). Fumbata – tendata (Ala. 1)

(d). Aliangua bendera baada ya kifo cha mfalme wao.(Ala. 1) (Tah: akipata kitenzi na aporonge kwingineko apate½)

(e). si - nafsi (kanusha) (½) ta -wakati (½)
ku -kikanushi cha wakati uliopita (½) pia -mzizi a -kishio (½) (ala.2)

(f). sikumkuta -ku (ala1)

(g). Ukielewana na mwalimu utapata amani siku zote shuleni. (ala. 2)

(i). Mwanangu - kitondo (ala.1) Kondoo -kipozi (ala. 1)

(j). “Ninataka kwenda sokoni” Mvulana alimwambia babake. (ala. 2)

(k). Masikio yangu si mazuri Sielewi unavyosema Mimi ni mgonjwa (zozote 2 al.2)

(l). Mwanagenzi/msomi/mkurufunzi ngeu (ala. 2) (m) ‘nne (ala.1)

(n). randa -kifaa cha seremala/surura/sawazisha mbao landa -fanana/shabihi/chukuana/landana (Tazi: Lazima mwanafunzi atunge sentensi mbili tofauti) (al.2)

(o). (i). Nimempa mwalimu mkuu kitabu . Nimempatia mwalimu mkuu kitabu. (al. 1) (yoyote moja ala. 1)

(ii). sahani iliyovunjika ni mpya. sahani yenye kuvunjika ni mpya. sahani mpya imevunjika. Sahani mpya ndiyo iliyovunjika. (al. 1) (yoyote moja ala.1)

(p). enda joshi – endelea/fanikisha/enda mbele (ala. 1) Hana hanani – asiye na chochote (ala. 1)

(q). (i). - /i/ (ala.1) (ii). - /s/ (ala. 1) (sauti ifungiwe au aiandike kama herufi ndogo ikiwa harufi kubwa asipate)

(r). kunguni- mofimu huru (ala. 1) Mgeni - m-kiambishi umoja geni –mzizi wa nomino (al.1)

MAKOSA

s- ondoa hadi nusu ya jumla ya alama ambazo mtahiniwa ametuzwa katika kisehemu.

h -kila kosa linapotokea mara ya kwanza hadi makosa 6 (al. 3)

30 marks

4. ISIMUJAMII (Alama 10)

4.

(a). Kimefanywa kuwa lugha ya taifa.

Hufunzwa kama somo la lazima shuleni.

Vyama vingi vimeundwa ili kushughulikia na kueneza Kiswahili (mf CHAKITA, CHAKIKE)

Vyombo vya habari na mawasiliano vimetumiwa kukuza na kusambaza Kiswahili k.m magazeti, vituo vya redio na runinga n.k.

Katiba ya nchi imekipa Kiswahili hadhi Kiswahili kinatumika katika mtandao.

Vitabu vingi vimechapishwa katika lugha ya Kiswahili .

Kiswahili kinatumika kama kigezo cha kuwachuja wanaojiunga na taaluma mbalimbali.

Kampeni za kisiasa huendeshwa katika Kiswahili.

Dini inaenezwa kupitia Kiswahili. (zozote 5 x 1 = 5)

(b). -Makosa katika matumizi ya lugha.

Wengi huyafanya kimakusudi kwa mfano wanasarakasi ili kuwatumbuiza watu.

-Athari za lugha ya kwanza Mf roo - roho Chika -shika

-Kutofahamu kanuni za lugha Mf watu wakumi

-Kutoelewa kaida za lugha kwa mf. Mzee kumsalimia mwanawe ‘shikamoo’

-Hali ya kiakili ya mtu Mf kutokana na ulevi

-Kuzungumza kwa haraka haraka (pengine kwa sababu ya hasira/furaha)

-Ujumuishaji wa kanuni za sarufi kwa mfano katika mnyambuliko. m.f: pungusha

- punguza kimbisha-kimbiza ungusha-unguza (zozote 4 al. 8) KUTUZA

- Maelezo yaambatane na mifano. MAKOSA:

s -makosa manne al.2

h – makosa manne al. 2

10 marks

Back Top