Search
Free School Management System
Free School Management System for Kenya

Free School Management System

Learn More

KCSE CLUSTER TESTS 26

Kiswahili Paper 3

SEHEMU YA A (Alama 20)

Riwaya-S. A. Mohamed: Utengano
1.

a) i) Maneno ya Biti kocho
ii) Anamwambia Bw maksuudi
iii) Nyumbani kwa Bw maksuudi
iv) Baada ya Bw maksuudi kutoka kwa Bi.kazija anakuta mkewe Bi Tamima amejifungua. Anampiga huku akimlaumu kwa kutoroka kwa Maimuna .

Biti kocho anaingilia kati kumzuia Maksuudi asiendelee kumchapa Bi Tamina
Biti anamlaumu Bw Maksuudi kwa unafiki wake kwa kusema huku nje wanawake wasitawishwe huku akiendelea kumtawisha mkewe
4x1=4


b) hapana asiyejua siasa dunia hii
i) Biti kocho anatetea uhuru wa mwanamke kutotawishwa
ii) Biti kocho anamlaumu Maksuudi kwa unafiki wake kutetea usawa katika mikutano lakini anatawisha mkewe na bintiye pale nyumbani
iii) Biti kocho na Farashuu wanamsaidia maimuna kuvunja minyororo ya utawa kwa kutoroka nyumbani
iv) Katika mkutano wa siasa uwanjani uhuru watu walisema wamechoka kudanganywa na wanasiasa kwa ahadi zisizowezekana
v) Mzee Bakari katika mkutano wa siasa anaelewa kuwa ahadi za zanga za kuwajengea njia n.k haziwezekani kwani nchi yao ni maskini
vi) Kazija anadhihirisha kasoro za maksuudi na zanga hadharani
vii) Umma kutaka kuwapiga zanga na maksuudi kwa sababu wanaelewa maovu wanayowafanyia
viii) Fadhili anakosana na kakake maksuudi kwa sababu hakubaliani na siasa za maksuudi za kudhulumu umma
zozote 4x2=8


c)
i)Mnenaji Biti kocho ni mwajiriwa wa Maksuudi
ii) Anajua kuwa amewatawisha mkewe na bintiye ingawa huko nje anapinga utawa wa wanawake
iii) Anaelewa kuwa maksudi anajifanya shehe ilhali anafanyia watu maovu
iv) Anajua maksuudi alivyomtesa Mwanasururu na kusababisha kifo chake
v) Anajua kuwa Maksuudi ni mpenzi wa Kazija
vi) Anajua mpango wao na Kazija wa kuwakutanisha Maksuudi na mwanawe Mussa kama waume wenza
vii) Amefaulu kumtorosha Maimuna kwa hivyo anajua hisia za Maimuna kumhusu Maksuudi
viii) Biti kocho anajua Maksuudi anavyowadhulumu wafanyakazi wake kwani yeye ni mmoja wao
ix) Anajua mateso anayomfanyia mkewe Bi. Tamina
zozote 4x2=8

20 marks

SEHEMU YA B (Alama 20)

Tamthilia-Kithaka wa Mberia: Kifo kisimani
2.

a) Muktadha
- Msemaji ni Mweke akiongea na Gege

- Wako katika majengo ya utawala wa Butangi

- Kumshawishi Gege akubali kumwangamiza Mwelusi
4x1=4


b) i) Kuozwa Alida
ii) Maisha yake yatapaa/ atakuwa kama ndege anayeishi juu ya mbuyu
iii) Atakuwa na heshima kubwa katika Butangi
iv) Atakuwa na mali K.M mashamba ya minazi, uvuvi n.k
zote 4x1=4


c) i) Kuchota maji kwa kipimo – siku tatu kwa wiki
ii) Watuhumiwa kutiwa gerezani
iii) Mateso kwa wafungwa gerezani – kupigwa, kutopewa chakula
iv) Mauaji
v) Watoto kunyang’anywa uwanja wa kuchezea
vi) Mapendeleo- Mtoto wa Kaloo kupewa kazi
vii) Athari za vita vya kikabila ( Balusi /Batuitui vilivyothaminiwa na serikali
viii) Raia kupigwa na askari
mtoto wa Chendeke , Andua
ix) Unyanyasaji – Mbutwe kutolipwa baada ya kutoa huduma kwa serikali
zozote 6x2=12

20 marks

SEHEMU YA C (Alama 20)

Hadithi fupi-K. W: Wamitila: Mayai waziri wa maradhi na hadilti nyingine
3.

3 a) Tuzo
i) Salome kukataa pesa ya Kibwana

ii) Salome kumdanganya Kibwana kuwa ndiye mshindi wa tuzo

iii) Walinzi wa rais kumsukuma Kibwana

iv) Profesa Dzori kumpa Salome tuzo ilhali aliyestahili kupewa ni Kibwana

v) Mwajiri wa kibwana kumpa mshahara mdogo Zozote 5x1=5


b) Pwaguzi
i) Salim kutoroka kijijini mwao
ii) Salim kumwibia kijuba
iii) Salim kuwaibia watoto
iv) Salim kuwaibia wanakijiji (waumini)
v) Shehe kijuba kuwapigia waumini bao badala ya kuwafunza dini
vi) Shehe kijuba kuchukua ‘sadaka’ kwa waummini akidai ni ya kugharamia chai ya watoto
zozote 5x1


c) Msamaria
i) Kizito kumgonga Likono kwa gari lake na kutaka kutoroka
ii) Kizito kutaka kumbebea Likono katika kiti cha nyuma kulikokuwa na jibwa lake
iii) Kizito kuondoka kwa kasi na kuwarushia watu matope
iv) Kizito kumpeleka Likoni katika hospitali ghali (GIPFEL)
V) Daktari wa Gipfel kuhitaji fedha kabla ya kumhudumia Likoni
vi) Daktari wa Gipfel kutaka Likono afanyiwe operesheni isiyostahili
vii) Kizito na rafikiye kukataa kugharamia matibabu ya Likono na kutoroka
viii) Waajiri kutotaka kumwajiri Rita bintiye Likono hata baada ya kuhongwa
ix) Walimu kuwatimua wanawe Likoni shuleni kwa kutolipa karo
x) Mwajiri wa Likoni kusimamisha mshahara wa Likono.
Zozote 5x1=5


d) Kachukua hatua nyingine
i) Mavitu kumwachisha mkewe kazi
ii) Mavitu kujiachisa kazi
iii) Mavitu kukatiza masomo ya wanawe
iv) Jirani mwajiri wa Mavitu kumpachika mimba bintiye Mavitu
v) Mwajiri wa Mavitu kumkopesha hela kwa hila na baadaye Mavitu kulazimika kummegea shamba lake
vi) Serikali kukomesha utoaji wa lishe kwa wanafunzi shuleni
vii) Askari wa chifu kushika mtoto na ng’ombe wa mavitu kwa kula miwa ya jirani.
viii) Nduguye shemeji (kala) kupigwa risasi na walinzi wa mwanasiasa Fulani.
Zozote 5x1=5


4 Picha tano
a) I) Mayai akinyonya ziwa la mamake

ii) Mayai na watoto wenziwe wakiwa uchi wakioga na kucheza ndani ya maji chafu

iv) Akipokea zawadi ya buku kubwa la shakespears complete works kutoka kwa mwakilishi wa British Council
v) Picha alizopigwa akiwa mwalimu
vi) Picha zilizomwonyesha akizindua majengo ya kuendeleza maradhi mbalimbali
vii) Picha alizopigwa akiwa na rafiki zake wasomali na wamanga wenye maduka na za waafrika zilizoonyesha sura za kijanja ambazo alizirarua
viii) Picha ya mwanawe marehemu ukombozi aliyefariki miaka minne iliyopita katika ajali ya barabarani
zozote 5x2=10
kutaja 1, kueleza 1


4 b) Matatizo yanayokabili nchi za Afrika kulingana na hadithi ya mayai waziri wa maradhi’
i) Uongozi mbaya

- Wananchi hawafaidiki na matunda ya uhuru

- Viongozi km. Mayai wana tamaa ya kujitajirisha

ii) Kutowajibika kwa viongozi wa kisiasa

- Viongozi wanajishughulisha na maswala ya kibinafsi na kutozingatia maswala ya kitaifa (matatizo ya wananchi).

iii) Ukosefu wa maendeleo

- Wananchi kuishi katika umaskini k.m wakulima

- Wizara nyingi ni za kuwadunisha wananchi

iv) Mfumo duni wa elimu

- Jina ‘wizara ya elimu na mchakamchaka’

- Kazi ya walimu inadharauliwa na walimu kupewa mishahara duni

- Migomo mingi ya walimu na wanafunzi

v) Ukoloni mamboleo

- Viongozi wanaoalikwa katika sherehe za uhuru ni ma DC na ma PC wa enzi za ukoloni mkongwe

- Wafanyakazi wananyanyaswa na kunyonywa na waajiri wao km. wakulima, walimu ilivyokuwa nyakati za ukoloni

vi) Imani ya ushirikina

- Mayai anapouona mzuka wa ukombozi anawalaumu wazee waliohudhuria mazishi ya mwanawe

- Mayai anafikiria kwenda Bagamoyo au Tanga kupata suluhisho la vioja anavyoshuhudia

vii) Ufisadi na uhalifu - Mayai anararua picha alizopigwa akiwa na rafiki zake wahalifu.

Zozote 5x2=10 Kutaja -1 Kueleza -1

20 marks

SEHEMU YA D (Alama 20)

Ushairi
4.

a) Ola vile nimekonda, jasadi nimepooza.
Ona vile ambavyo mwili wangu umekonda na kupooza| kwisha nguvu | kuwa mnyonge 1x2=2
b) Umuhimu wa kipokeo: Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda

i) Kimalizio cha ubeti

ii) Msisitizo wa ujumbe wa mashairi 2x1=2

c) Sifa za kiarudhi ubeti 3 i) Mishororo minne ii) Vipande viwili iii) Mizani:

8: 8
8: 8
8: 8
8: 8
iv) Vina:

nda : za Nda : za

Nda: za Za : nda 4x1=4

d) Methali : cha kuvunda hakina ubani 1x2=2

e) Maudhui ubeti -2

Mshairi anaongea kuhusu mpenzi wake aliyempenda kama embe.

Anasema kuwa mpenzi huyo alimgeuka na kukosa shukrani vile punda afanyavyo.

Anamsihi mpenzi wake aondoke badala ya kuendelea kumtesa 1x2=2

f) Sauti ya mpenzi wake ambayo ni nzuri kama ya kinanda 1x1=1
h) i) Mayaza – shida |matatizo |mateso |tabu
ii) gwanda – nguo |mavazi
iii) Kuwanda – kunenepa 3x1=3

20 marks

SEHEMU YA E (Alama 20)

Fasihi simulizi
5.

6 a) Ni hali ambapo watendaji huiga na kutenda matendo ya watu au viumbe katika jamii
1x2=2
b) i) Matendo ya kweli yanayotokea katika jamii hutendeka katika mazingira halisi na washiriki huwa ndio hadhia. Maigizo ya aina hii haya hitaji jukwaa au vifaa maalum
ii) Maigizo ya mambo nje ya mazingira, mkutadha, wakati na mahali halisi
2x2=4


c) Sifa zozote TANO za maigizo
i) Huwa na wahusika maalum
ii) Huwa na vitendo vingi tofauti
iii) Hutendwa mbele ya hadhira
iv) Hutumiwa maleba, mapambo na vifaa kuzua mazingira maalum
v) Wahusika hufanya mazoezi kabla ya maigizo halisi
vi) Pengine hutumia ishara
zozote 5x2=10


d) Dhima nne
i) kukuza maadili
ii) kuburudisha
iii) kuwapa watu maarifa na stadi mbalimbali / kuelimisha
iv) kuimarisha lugha
v) kukuza vipawa
zozote 4x1=4


7 a i) Njia tatu za ukusanyaji wa data
i) Kutumia hojaji

ii) Mahojiano

iii) Kushiriki moja kwa moja

iv) Kutazama |kushuhudia

v) Maandishi- kusoma makala juu ya tanzu husika

vi) Kunasa sauti

vii) Filamu na video Zozote 3x1=3


ii) Mbinu tatu za kuhifadhi fasihi simulizi
i) Maandishi

ii) Kanda za kunasia sauti |kanda za video na filamu – yaani vifaa meme

iii) Akili ya binadamu

iv) Maumbile na mazingira k.m kwa nini fisi huchechemea n.k v) Michoro Zozote 4x1=4


Umuhimu wa kuhifadhi fasihi simulizi
i) Kuelimisha
ii) Kuelekeza/ kushauri

iii) Kuonya | kutahadharisha

iv) Kuburudisha

v) Kufikirisha

vi) Kukuza utamaduni

vii) Kueleza historia Zozote 3x1=3


b) i) Maana ya ushauri
Ni tungo ambazo hutumia lugha fupi, ya mkato na iliyopangwa kwa utaratibu Fulani
1x1=1
ii) i) kifunga nyama
- Mashairi ya kimafumbo yaliyofumbwa ili washairi wengine wayafumbue 1x2=2
ii) Waadhi
- Ushairi wa kutoa mawaidha 1x2=2
iii) Sifa za ushairi simulizi
i) Asili yake ni nyimbo ambazo hazikufuata utaratibu maalum

ii) Huelezea hisia za ndani za mtu

iii) Hutumiwa kuchochea hisia, kumzindua na kumwathathiri anayeusikiliza

iv) Huwa na pande mbili – msimulizi na msikilizaji

v) Hutumiwa katika mazingira tofauti

vi) Maudhui yake yanalingana na mazingira yaliotungiwa shairi km ndoa, jando n.k

vii) Hubuniwa papo hapo na kuwasilishwa kwa hadhira

viii) Unaweza kuwasilishwa ukiambatana na ala za muziki

ix) Hutumia lugha ya kitamathali Zozote 5x1=5

20 marks

Back Top