Kiswahili Paper 3 Question Paper
KCSE CLUSTER TESTS 26
Kiswahili Paper 3
SEHEMU YA A (Alama 20)
Riwaya-S. A. Mohamed: Utengano
LAZIMA
“Kumbe bwana wewe mjinga eeh. Yupo mtu asiyejua siasa dunia hii? Wandanganye hao wasiokujua, mimi nakujua vilivyo.”
a) Eleza muktadha wa dondoo hili (alama 4)
b) Onyesha inavyodhihirika kuwa hapana asiyejua siasa dunia hii (alama 8)
c) Thibitisha kuwa mnenaji anamjua mnenewa vilivyo (alama 8)
20 marks
SEHEMU YA B (Alama 20)
Tamthilia-Kithaka wa Mberia: Kifo kisimani“Bahati nasibu inapomteremkia mtu, mara nyingine uhalisia huonekana kama ndoto,
mambo huwa hayaeleweki kwa urahisi’’
i) Fafanua muktadha wa dondoo hii. (alama 4)
ii) Onyesha bahati inayorejelewa katika dondoo hii. (alama 4)
iii) Eleza jinsi ambavyo watu wengine katika tamthlia walikosa kuteremkiwa na bahati nasibu (alama 12)
20 marks
SEHEMU YA C (Alama 20)
Hadithi fupi-K. W: Wamitila: Mayai waziri wa maradhi na hadilti nyingineJibu swali la 3 au la 4
3. ‘Kweli ibilisi wa mtu ni mtu! Thibitisha kauli hii kwa kurejelea hadithi zifuatazo (alama 20)
i) Tuzo
ii) Pwaguzi
iii) Msamaria
iv) Kachukua hatua nyingine
4 “……………Katika ukurasa huu aliona picha ya mamake……………………..’’
i) Mbali na picha hii, eleza picha nyingine tano alizoziona. (alama10)
ii) Hadithi ‘Mayai waziri wa maradhi’ inamulika matatizo mbalimbali yanayozikabili nchi nyingi za kiafrika. Thibitisha kauli hii kwa kufafanua matatizo yoyote matano. (alama 10)
20 marks
SEHEMU YA D (Alama 20)
Ushairi
5. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali
Wangu niliyekupenda, leo nitakufukuza
Kuishi umenishinda, waniletea mayaza
Ola vile nimekonda, jasadi nimepooza
Uwache kuniumiza,ni heri mwana kunenda
Ulikuwa wangu nyonda, huba nikaikoleza
Kukupenda kama tunda, embe lenye uliwaza
Ukajigeuza punda, teke umenicharaza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
Nimekonda kama ngonda, mwandani wanilemaza
Sautiyo ya kinanda, sitaki kusikiliza
Sikutaki bora kwenda, muhibu wanishangaza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
Mengi ulionitenda, si madogo yakupuza
Nalikupa kila gwanda, uvae na kupendeza
Ulikula na kuwanda, kadiri ulivyoweza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda.
Kinyume ulipokwenda, nilidhani kuteleza
Na wewe hukujilinda, nyendo mbaya kupunguza
Cha kuvunda kisha vunda, hata ukikifukiza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
Mja wewe wanishinda, kwa tama wachukiza
Kila kitu unadanda, kingawa cha kuumiza
Huwi ndani ya kibanda, huishi kujitembeza
Uwache kuniumiza, ni heri mwana kunenda
a) Eleza maana ya mleo wa ubeti wa kwanza (alama 2)
b) Fafanua umuhimu wa kipokeo cha shairi hili (alama 2)
c) Eleza sifa za kiarudhi katika ubeti wa tatu (alama 4)
d) Taja methali inayodokezwa katika ubeti wa tano wa shairi hili (alama 2)
e) Eleza maudhui ya ubeti wa pili wa shairi hili. (alama 2)
f) Ni jambo lipi zuri ambalo mshairi atalikosa? (alama 1)
g) Andika ubeti wa sita wa shairi hili katika lugha nathari (alama 4)
h) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi . (alama 3)
i) Mayaza
ii) gwanda
iii) Kuwanda
20 marks
SEHEMU YA E (Alama 20)
Fasihi simuliziJibu swali la 6 au 7
6 a) Ni nini maana ya maigizo katika fasihi simulizi. (alama 2)
b) Fafanua aina mbili kuu za maigizo (alama 4)
c) Taja sifa zozote tano za maigizo. (alama 10)
d) Eleza dhima zozote nne za maigizo (alama 4)
7 a) i) Taja njia zozote tatu za ukusanyaji wa data katika fasihi simulizi. (alama 3)
ii) Taja mbinu zozote tatu zinazotumiwa kuhifadhi fasihi simulizi huku ukionyesha umuhimu wa kuhifadhi fasihi hii. (alama 7)
b) Eleza maana ya ushairi kwa mujibu wa fasihi simulizi. (alama 1)
ii) Ni nini maana ya mashairi yafuatayo. (alama 4)
i) Mashairi ya kifunga nyama
ii) Waadhi
iii) Eleza sifa za ushairi simulizi (alama 8)
20 marks